• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya muleba
    • Dira na Dhima
    • Core Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Mali asili
      • Ugavi
      • TEHEMA
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utumishi
      • Fedha
      • Mipango na Uchumi
      • Maji
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo/Umwagiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ratiba
  • Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
  • Miradi
    • Itakayo- Tekelezwa
      • Inayo-Endelea
      • Iliyo-Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za ofisini au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Makitaba ya Picha

UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIMEYA WAPIGA HATUA

Imewekwa : May 26th, 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Ndg. Emmanuel Sherembi ametembelea na kukagua shughuli za ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya Kimeya ili kuona maendeleo ya ujenzi huo unaotakiwa kukamilika ifikapo tarehe 31/05/2018.

Akikagua ujenzi huo, Ndg. Emmanuel Sherembi amewasisitiza mafundi waliopewa kazi za ujenzi wa kituo hicho kukamilisha kazi zilizobaki kwa wakati. Na kuwataka wafanye kazi mchana na usiku ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi ndani ya muda waliopewa.

"Zimebaki siku chache mkabidhi kazi hii, tuliona ni vema tuweke umeme ili muweze kufanya kazi mchana na usiku hivyo nategemea nikirudi hapa tarehe 31/05/2018 nitakuta kazi hii imekamilika" alieleza Ndg. Emmanuel Sherembi.

Kituo cha Afya Kimeya ni miongoni mwa vituo 139 vya awamu ya pili ambavyo kila kituo kilipewa kiasi cha shilingi milioni 400 kutoka serikali kuu kwa ufadhili wa World Bank kwa ajili ya upanuzi wa vituo na hadi sasa chumba cha upasuaji (Theatre), Wodi ya Akina mama, Nyumba ya mtumishi, Maabara na Chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) vyote vipo katika hatua ya umaliziaji.

Ujenzi huu umetekelezwa na mafundi wanaopatikana katika maeneo ya wananchi na kila jengo linafundi anayejitegemea ili kusaidia kukamilishaujenzi huu kwa muda uliopangwa. Aidha, ujenzi huu unasimamiwa na Kamati ya Ujenzi iliyotokana na bodi ya Kituo cha Afya kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ambao ni Mhandisi wa Ujenzi, Afisa Manunuzi, Mganga Mkuu na Afisa Mipango.

Ujenzi ulianza mnamo mwezi Februari, 2018 na unatakiwa ukamilike kufikia tarehe 31/05/2018 kama ambavyo Serikali imeagiza.

Matangazo ya kawaida

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA BWENI,UFUNDI NA SHULE MAALUM December 18, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA KUTWA KIDATO CHA KWANZA December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIMEYA WAPIGA HATUA

    May 26, 2018
  • MAPATO YA NDANI YAIMARISHA VITENDEA KAZI

    May 25, 2018
  • WAZEE WETU FAHARI YETU

    May 04, 2018
  • TUMLINDE MTOTO WA KIKE NGUVU KAZI YA TAIFA LA KESHO

    April 23, 2018
  • Angalia zote

Video

Hotuba ya jana ya Rais akiwa nchini Kampala
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ajira
  • Kagera
  • Immigration

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais- UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kagabiro

    Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera

    Simu: +255 (28) 222-4013

    Simu: +255-756-350-183

    Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz

Mawasiliano mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa